Swahili

Anti-Discrimination NSW (Shirika la Kupambana na Ubaguzi la NSW)

Sisi ni shirika la serikali ya jimbo la New South Wales linalotekeleza Anti-Discrimination Act 1977 (Sheria ya Kupambana na Ubaguzi 1977) (Sheria). Tunatoa huduma bila malipo na tunajitahidi kuondoa ubaguzi katika New South Wales kwa:

  • kujibu maswali
  • kukusanya malalamiko
  • kuhamasisha kuhusu ubaguzi na athari zake
  • kusimamia maombi ya msamaha wa sheria kutolewa ili kuruhusu kupendelea vikundi kadhaa vya watu kuboresha ufikiaji wa baadhi ya kazi, mipango, huduma au vifaa
  • kuishauri serikali kuhusu masuala ya ubaguzi.

Ubaguzi ni nini?

Ubaguzi ni pale mtu anapokosa kutendewa haki kwa sababu ana sifa, au anadhaniwa kuwa na sifa ambayo inalindwa na sheria ya New South Wales.

Sifa hizi ni pamoja na:

  • ulemavu (inajumuisha magonjwa na maradhi)
  • jinsia (inajumuisha ujauzito na hali ya unyonyeshaji)
  • rangi
  • umri
  • hali ya ndoa au uchumba
  • ushoga
  • kuwa na jinsia mbadala
  • majukumu ya mtunzaji.

Ni kinyume cha sheria kuwa na ubaguzi katika sehemu fulani za umma. Hizi ni pamoja na:

  • maeneo ya kazi
  • miktadha ya elimu
  • mahali bidhaa na huduma hutolewa
  • mahali penye makazi
  • katika vilabu vilivyosajilwa.

Ubaguzi wa majukumu ya mtunzaji ni kinyume cha sheria kazini.

Unyanyasaji wa kingono

Ni kinyume cha sheria kumnyanyasa mtu kwa kingono. Unyanyasaji wa kijinsia ni tabia yoyote isiyokubalika ya kingono ambayo inamfanya mtu ahisi kukerwa, kudhalilika au kutishwa.

Hizi ni pamoja na:

  • kumtongoza mtu
  • kuomba ngono
  • ishara, mizaha au maoni ya kingono.

Matamshi ya chuki

Matamshi ya chuki ni hatua ya umma inayoweza kusababisha chuki, dharau au dhihaka kwa mtu au kundi la watu. Ni kinyume cha sheria kutoa matashi ya chuki kuhusu sifa fulani.

Sifa hizi ni pamoja na:

  • rangi
  • dini
  • ushoga
  • kuwa na jinsia mbadala
  • kuwa na Virusi vya UKIMWI/UKIMWI.

Kitendo chochote cha umma kinachotishia au kuchochea dhuluma kwa kundi la watu kwa sababu ya rangi, imani yao ya ushirika, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa jinsia, kuwa ngono au kuwa na jinsia zote au kuwa na Virusi vya UKIMWI ni kosa la jinai ambalo linapaswa kupelekwa kwa polisi.

Uonevu

Ikiwa umedhulumiwa kwa sababu umefanya (au unapanga kutoa) malalamiko ya ubaguzi, au kwa sababu umetoa taarifa au ushahidi juu ya malalamiko ya ubaguzi, inajulikana kama uonevu. Uonevu ni kinyume cha sheria katika jimbo la New South Wales.

Unachopaswa kufanya unapobaguliwa

Wasiliana na huduma ya usaidizi ya Anti-Discrimination NSW (Shirika la Kupambana na Ubaguzi la NSW) kwa 02 9268 5544 au 1800 670 812, au tuma barua pepe kwa adbcontact@justice.nsw.gov.au. Unaweza kuwasiliana nasi hata ikiwa huna hakika ikiwa hali yako au kile kilichokupata ni kinyume cha sheria, au ikiwa ungependa kupata taarifa kuhusu sheria za kupambana na ubaguzi ya NSW.

Ukibaguliwa, kunyanyaswa au kupokea matamshi ya chuki na ungependa kutoa malalamiko rasmi juu ya mtu au kampuni, tafadhali tumia fomu yetu ya malalamiko. Unaweza kuandika malalamiko yako kwa lugha yoyote na tutatafsiri malalamiko yako kwa Kiingereza bila malipo yoyote. Tuma malalamiko yako kwa complaintsadb@justice.nsw.gov.au. Ikiwa unatatizika kuandika malalamiko yako, unaweza kuwasiliana nasi ili tujadili chaguo zingine za kuwasilisha malalamiko yako.

Ikiwa unahitaji mkalimani kupata huduma zetu zozote, tafadhali wasiliana na Translating and Interpreting Service (Huduma ya Utafsiri na Ukalimani) kwa nambari 131 450 na uwaombe wapigie simu Anti-Discrimination NSW (Shirika la Kupambana na Ubaguzi la NSW) kwa 02 9268 5544.

Ikiwa unahitaji usaidizi wa kisheria, wasiliana na Law Access (Ufikiaji wa Sheria) kwa 1300 888 529.

Ikiwa umebaguliwa au umepokea matamshi ya chuki ambayo ni ya jinai, tafadhali wasiliana na Polisi wa NSW.

Ni nini kitatokea unapowasilisha malalamiko katika Anti-Discrimination NSW (Shirika la Kupambana na Ubaguzi la NSW)?

Jukumu letu ni kukusaidia wewe na mshtakiwa kupata suluhisho. Tunapopokea malalamiko yako, ikiwa inaonekana ni hali ambayo ni kinyume na sheria, tutayawasilisha kwa hatua inayofuata.

Tutawasiliana nawe kwa simu au barua ndani ya wiki mbili za kupokea malalamiko yako. Tutakapowasiliana nawe, tunaweza kukuuliza kuhusu taarifa nyingine yoyote tutakayohitaji. Pia, tutajadili jinsi tunavyopanga kushughulikia malalamiko yako.

Mtu unayelalamika anaitwa mshtakiwa. Tutamtumia mshtakiwa nakala ya malalamiko yako na hati yoyote uliyoyatoa, pamoja na barua kutoka kwetu ikielezea sheria husika. Kisha mshtakiwa atapata fursa ya kujibu.

Ikiwa hatua hii haitatatua hali hiyo, tunaweza kuwa na mkutano kati yako na mshtakiwa. Hatua hii inaitwa mkutano wa upatanisho. Upatanisho ni fursa ya pande zote mbili kuja pamoja na kujadili njia za kutatua malalamiko.

Hatuwezi kuegemea upande mmoja au kukupa ushauri wa kisheria. Ikiwa hatuwezi kukusaidia kutatua jambo hilo, unaweza kupeleka malalamiko yako kwenye NSW Civil and Administrative Tribunal (Mahakama ya Umma na Utawala ya NSW).

Pakua fomu ya malalamiko

Muhtasari wa Kupambana na Ubaguzi NSW

Mchakato wa malalamiko katika Kupambana na Ubaguzi NSW

Last updated:

24 Jan 2024

Was this content useful?
We will use your rating to help improve the site.
Please don't include personal or financial information here
Please don't include personal or financial information here

We acknowledge Aboriginal people as the First Nations Peoples of NSW and pay our respects to Elders past, present and future. We acknowledge the ongoing connection Aboriginal people have to this land and recognise Aboriginal people as the original custodians of this land.

Top Return to top of page Top